1985 - 2008
KARIBU KWENYE SHULE YA UMISHENI
KWA LUGHA YA KISWAHILI
na Mch. Paul Sungro Lee
Karibu Kwenye Shule Ya Umisheni Katika Lugha Ya Kiswahili
Orodha Ya
Masomo Kwa Lugha Ya Kiswahili Bila Malipo
Maswali Yaulizwayo Mara Kwa Mara
Kijitabu cha maelekezo kwa wanafunzi, viongozi wa kozi, na wachungaji
Karibu kwenye tovuti ya Kiswahili ya Shule ya Umisheni
Kasisi Silas Yego, Makamu wa
Askofu wa Africa Inland Church alisema, “Hitaji la Afrika leo
ni kupata viongozi wasomi”. Naye Dk. Tite Tienou, Kasisi
Kiongozi katika taasisi ya Trinity Evangelical Divinity School aliwahi
kusema, “Mbinu za sasa za ufundishaji hazina uwezo wa
kukabiliana na hitaji la uongozi katika kanisa la Afrika leo. Afrika
inahitaji walimu zaidi”. Shuhuda hizi ni moja tu ya mambo
yaliyotusukuma kutafsiri mafunzo haya kwa lugha ya Kiswahili.
Tafsiri hii ya Kiswahili ilifanywa na kikundi cha watumishi waaminifu
wa injili nchini Kenya kwa lengo moja la msingi; kuwafundisha
washuhudiaji na waanzilishi wa makanisa hapa Afrika katika siku hizi za
mwisho. Katika shughuli zangu za kikristo kwenye eneo la kuwaelimisha
wahudumu, nilikuwa na ndoto ya kupata muhtasari wenye mafunzo yote
muhimu yanayohitajika ili kumwandaa mhubiri kwa ajili ya huduma. Baada
ya kupata ujuzi fulani kuhusu namna ya kuwaelimisha wahudumu na kazi ya
kuanzisha makanisa katika eneo la Afrika Mashariki kwa miaka kadhaa,
nilianza kuelewa kwamba panahitajika kiwango kikubwa zaidi cha juhudi
za kuwaandaa wahubiri kwa ajili ya Afrika; mawazo ambayo
hayakutofautiana na yale ya viongozi wengine wa kikristo niliowataja
hapo juu. Miaka kadhaa iliyopita, Mungu aliniongoza kugundua mpango wa
masomo kama ulivyoandikwa na Dk. Les Norman wa DCI Trust huko Uingereza.
Mpango huu wa masomo tuliupokea na kuufanya sehemu ya mkakati wetu wa
mafunzo hapa Afrika Mashariki, na umetusaidia kuyafanya makanisa
yaliyokuwapo kuanzisha makanisa mengine kwa kuwapa mafunzo viongozi
muhimu katika makanisa yao. Ni wazi kwamba huu mkakati wa Shule ya
Umisheni umekuwa ni uti wa mgongo wa huduma yetu ya kuanzisha makanisa
tangu mwaka 2000. Mimi na wenzangu wengi tumekubali kwamba hii ilikuwa
ni kazi ya Mungu kwa jinsi tulivyoona mkakati huu ukichangia kuanzishwa
kwa makanisa mapya yapatayo 150 katika kipindi kifupi tu cha miaka
mitatu.
Ndipo baadaye tukabaini kwamba iwapo masomo haya yatatafsiriwa katika
lugha ya Kiswahili, kutakuwa na ongezeko la viongozi wa kanisa wasomi,
na waanzilishi wa makanisa wanaofahamu vizuri Kiswahili. Baada ya
tafsiri hiyo kukamilika, na kama ilivyotarajiwa, kulikuwako na ongezeko
la makanisa mapya katika maeneo ya umisheni wetu. Tunaweza kukushuhudia
uweza ya mafunzo haya; unatenda kazi kwelikweli katika huduma yetu!
Ni matumaini yetu kwamba utafurahia mafunzo haya kwa lugha ya
Kiswahili. Tafadhali yapitie, na iwapo utahitaji taarifa zaidi baada ya
kutembelea tovuti yetu, basi usisite kuwasiliana nasi kwa anwani
ifuatayo: eaptc@eaptc.org
Tutafurahi kukujibu kwa haraka iwezekanavyo.
Kwa mara nyingine napenda kumshukuru kwa moyo wa dhati Dk. Les Norman
kwa kuandaa masomo haya. Namshukuru pia kwa kututia moyo wakati
tulipokuwa tukifanya kazi ya kutafsiri. Shukrani nyingi zaidi namtolea
Bwana Yesu aliyeniita kwenye huduma hii ya ajabu, na kazi ya maana
– kuwatumikia watumwa wake!
Karibu Kwenye Shule Ya Umisheni Katika Lugha Ya Kiswahili
Orodha Ya
Masomo Kwa Lugha Ya Kiswahili Bila Malipo
Maswali Yaulizwayo Mara Kwa Mara
Kijitabu cha maelekezo kwa wanafunzi, viongozi wa kozi, na wachungaji
With many thanks to Pastor Dastan Mboera,
Dar es Salaaam, Tanzania
for this revision and translation from the original English
mboeradsk @ yahoo.com
1985 - 2007
www.dci.org.uk